1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRAZIL,INDIA NA AFR.KUSINI

11 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFY1

DURBAN:

Zikihisi kwamba nchi zinazoinukia zinahitaji mfumo sawa wa kibiashara,India,Brazil na Afrika Kusini zimeapa kufanya juhudi kuimarisha mafungamano ya biashara na raslimali kati yao .

Hii amesema waziri wa nje wa India K.Natwar Singh katika mkutano wa Tume ya nchi hizo tatu huko Durban,Afrika Kusini.

Aliongeza kusema wana furaha kuona nchi zao 3 zimechangia mno katika kuyaongoza majadiliano ya Shirika la Biashara Duniani (WTO).Akasema waziri huyo wa nje wa India,

"Kwa kadiri tunazungumza kwa sauti moja,ndipo tunapozidi kuwa na uzito katika maswali ya kilimwengu.

Waziri wa nje wa Afrika Kusini,Nkosazna Dlamini-Zuma amesema nae kwamba nchi hizi 3 zikiwa na kituo maalumu kijiografia katika mabara 3,yatabakia yameungana kabla kufanyika mazungumzo ya shirika hilo la Biashara Duniani huko Hong Kong hapo desemba, mwaka huu.

Mara tu baada ya kuwasili kwake mjini Cape Town jana, Natwar Singh alikagua uhusiano kati ya India na Afrika kusini katika mazungumzo na Dlamini-Zuma.