1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brazil, Nikaragua zafukuziana mabalozi

9 Agosti 2024

Brazil na Nikaragua zimefukuziana mabalozi wao katika mkasa unaotazamwa kama ulipizianaji kisasi baina ya serikali za nchi hizo zilizowahi kuwa washirika wakubwa wa siasa za mrengo wa kushoto.

https://p.dw.com/p/4jHde
Daniel Ortega und Luiz Inacio Lula da Silva
Picha: Evaristo Sa/AFP/Getty Images

Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil aliamua kumfukuza balozi wa Nikaraguwa mjini Brasilia, baada ya Rais Daniel Ortega wa Nikaragua kumuamuru mwakilishi wa Brazil kuondoka mjini Managua.

Hatua hii inadhihirisha mzozo mkubwa uliopo kati ya Lula na baadhi ya serikali za mrengo wa kushoto barani Amerika Kusini ulioongezeka kutokana na matokeo ya uchaguzi wa Venezuela.

Sababu nyengine inayotajwa ni hatua ya Rais Lula kuingilia kati kwa ombi la Mkuu wa Kanisa Katoliki Papa Francis, akitaka mkosoaji mkubwa wa Rais Ortega kuachiwa huru kutoka jela.