1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brazil na Ubelgiji watinga robo fainali

3 Julai 2018

Katika michuano ya kuingia robo fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi, Brazil imeichapa Mexico 2-0 na hivyo kujipatia tiketi ya kuingia duru inayofuata. Nayo Japan yatolewa na Ubelgiji baada ya kufungwa 2-3.

https://p.dw.com/p/30jfG
Wachezaji wa timu ya taifa ya Brazil
Picha: Reuters/M. Dalder

Kocha wa Japan Akira Nishino amekiri kusikitishwa baada ya kikosi chake kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi, kufuatia kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Ubelgiji. Amesema hakutarajia kupigo hicho, baada ya Nacer Chadli wa Ubelgiji kutia wavuni bao la ushindi katika dakika ya 94 ya mchezo huo, hivyo kuzima kabisa ndoto za Japan kuingia katika hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hiyo. Brazil nayo imeondoka na ushindi mnono wa mabao 2-0 dhidi ya Mexico, ambayo pia imeyaaga mashindano hayo. Brazil sasa itakutana na Ubelgiji kwenye mchezo unaotabiriwa kuwa utakuwa mgumu katika hatua ya robo fainali.  

Mchezaji Takashi Inui wa Japan
Mchezaji Takashi Inui wa JapanPicha: Reuters/J. Silva