1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bonn. Rais wa Ujerumani atembelea Deutsche Welle.

8 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CClQ

Rais wa Ujerumani Horst Köhler leo amezuri jumba la utangazaji la Deutsche Welle, akipokewa kwa shangwe na nyimbo kutoka kwa wafanyakazi wa idhaa ya Kiswahili na idara nyingine mara alipowasili.

Akizungumza na mkurugenzi mkuu wa Deutsche Welle Erik Bettermann na mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi wa shirika hilo, valentin Schmidt, rais Köhler ameonyesha kuwa rafiki wa kituo cha matangazo ya nje ya radio hiyo. Amesema kuwa Ujerumani inasifa duniani ya kuwa na haki na uaminifu na hivyo Deutsche Welle pia inajumuishwa.