1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BOMBAY: Mafuriko yamesababisha vifo nchini India

27 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEqL

Mvua kubwa zilizosababisha mafuriko na mmomonyoko wa ardhi,zimeuwa darzeni kadhaa ya watu katika jimbo la Maharashtra magharibi mwa India.Maafisa wamesema watu wengi bado wanakosekana na makundi ya wasaidizi yanahamisha maelfu ya watu walionasa kwa sababu ya maji yanayozidi kupanda juu katika mji mkuu wa biashara Bombay.Vikosi vya angani,ardhi kavu na vya wanamaji pia vimeombwa msaada.Kwa siku ya pili hii leo wakaazi hawana umeme wala mawasiliano ya simu.Maafisa wamesema wana wasiwasi kuhusu hatima ya kiasi ya watu 150 wanaokhofiwa kuwa wamegubikwa na ardhi iliyomomonyoka katika kijiji kimoja kusini mwa Bombay.Siku ya jumanne mji wa Bombay ulishuhudia mvua kubwa kabisa tangu muda wa zaidi ya miongo mitatu.Imetabiriwa kuwa katika kipindi cha saa 48 zijazo kutanyesha mvua kubwa sana na kutapiga upepo mkali.