1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken aelezea matumaini ya kusitishwa vita huko Sudan

21 Agosti 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ameelezea matumaini yake kwamba, makubaliano yaliyofikiwa ya kutolewa kwa misaada ya kiutu Sudan, yanaweza kuwa chanzo cha makubaliano ya kuvimaliza vita nchini humo.

https://p.dw.com/p/4jiuK
Qatar | Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwasili
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akizungumza na waandishi wa habari, huko Doha, Qatar, Agosti 20, 2024Picha: Kevin Mohatt/REUTERS

Blinken ambaye anafanya ziara Misri na Qatar kwa lengo kuu la kutafuta usitishwaji wa mapigano katika vita vya Gaza, amesema ameulizia pia kuhusiana na mazungumzo yanayoongozwa na Marekani kuhusiana na Sudan yanayoendelea nchini Uswisi. Amewaambia waandishi wa habari kwamba Sudan kwa sasa ndiyo inayoshuhudia hali mbaya zaidi ya kiutu duniani. Mjumbe mkuu wa Marekani nchini Sudan Tom Perriello amesema atakutana na ujumbe wa serikali ya Sudan katika hatua yake ya hivi karibuni ya kujaribu kuwarai washiriki mazungumzo yanayoendelea Uswisi.