Bielfeld na Hertha, kuingia vitani katika Bundesliga
5 Februari 2009Kwa Hertha Berlin ambayo ina pointi 36 ikiwa katika nafasi ya nne iwapo itashinda hii leo itafikisha pointi 39 na hivyo kukamata usukani wa Bundesliga unaoshikiliwa na timu ya kijijini iliyopanda daraja msimu Hoffeinheim yenye pointi 38.
Hertha katika mechi yakeJumamosi iliyopita iliichapa Eintacht Frankfurt mabao 2-1 ambapo mabao yote mawili yaliwekwa wavuni na mshambuliaji wake hatari Marko Pantelic.
Lakini hata hivyo mshambuliaji huyo leo hatakuwa uwanjani kutokana na mauamivu.
Macho lakini yatakuwa kesho Jumamosi ambapo Schalker 04 na Werder Bremen zitapepetana, lakini katika hali tofauti na misimu iliyopita ambapo timu hizo zilikuwa katika kupigana kumbo kuwania ubingwa.
Kwa misimu kadhaa vilabu hivyo vimekuwa vikitisa Bundesliga na kuwa washindani wakubwa wa ufalme wa kandanda Ujerumani, lakini msimu huu timu hizo zinaonekana kupepesuka na zaidi zitakuwa zikipigana kumbo si kuwania ubingwa bali kutoshuka daraja na angalau kupata nafasi ya kucheza katika michuano ya UEFA msimu ujayo.
Bremen ambayo ilitwaa ubingwa mwaka 2004, haijawahi kumaliza ligi ikiwa nje ya nafasi tatu za juu kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, ambapo Schalke kwa upande wake imekuwa katika nne za juu katika kipindi cha miaka minne iliyopita mfululizo.
Werder Bremen hivi sasa inakamata nafasi ya kumi na iwapo itapoteza mechi yake hii leo, huenda majaaliwa ya kocha wake Thomas Schaaf yakawa katika kiza kinene.
Hata hivyo mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo Klaus Allofs ametupilia mbali pendekezo lolote la kumtupia virago Thomas Schaaf ambaye mwezi Mei mwaka huu atafikisha miaka kumi toka ajiunga na timu hiyo.
Amesema kuwa bado hata hivyo Bremen ina nafasi ya kufanya vyema katika michuano ya kombe la shirikisho la soka la Ujerumani, pamoja na ile ya UEFA ambapo timu hiyo inashiriki.
Kwa upande wa Schalke timu hiyo iko katika kipindi cha mpito mtu waweza kukiita kwani inajaribu kujenga timu mpya ya vijana chini ya kocha wake Mholanzi Fred Rutten.
Wakati Bremen na Schalke wakipepesuka uzani wa umwamba katika Bundesliga hivi sasa umeahamia kwengine, ambapo wanakijiji wa Hoffenheim waliyoivamia Bundesliga kwa kishindo kikubwa watakuwa ugenini huko Monchengladbach kuumana na Borrussia iliyoko mkiani
Hamburg inayokamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi 36 watakuwa ugenini kuumana na Karlsruhe.
Wakati huo huo Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Loew amemuita kundini kiungo chipukizi mwenye kipaji cha hali juu Mesut Oezil anayechezea Werder Bremen pamoja na kuwarejesha nahodha Michael Ballack na Torsten Frings kwa ajili ya pambano la kirafiki la kimataifa Jumatano ijayo dhidi ya Norway.
Mwaka jana Ballack alimkosoa kocha huyo juu ya mbinu zake za kutompa nafasi Frings, hatua ambayo iliwaingiza katika uhasama kabla ya kusuluhishwa.
Katika kikosi hicho Joachim Loew, amemuita beki asiye na mzaha wa timu ya kijijini ya Hoffenheim Andreas