1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Ushindi wa Ukraine na Israel ni muhimu kwa Marekani

20 Oktoba 2023

Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza kuwa kufanikiwa kwa Ukraine na Israel katika vita vyao ni muhimu kwa usalama wa Marekani. Biden amewasilisha hoja ya kuhusika zaidi kwa Marekani katika migogoro hiyo miwili

https://p.dw.com/p/4XnCR
Rais wa Marekani Joe Biden akitoa hotuba kutoka ofisi yake katika Ikulu ya Marekani Oktoba 19, 2023
Rais wa Marekani Joe BidenPicha: Jonathan Ernst/AFP

Katika hotuba ya nadra kutoka ofisini kwake katika ikulu ya Marekani Biden amesema ikiwa uchokozi wa kimataifa utaruhusiwa kuendelea, migogoro na machafuko inaweza kuenea katika sehemu nyingine za dunia.

Biden afananisha shambulio dhidi ya Israel na miezi 20 ya vita nchini Ukraine

Biden amesema kwamba shambulio dhidi ya Israel linalingana na takriban miezi 20 ya vita, mikasa na ukatili waliofanyiwa watu wa Ukraine. Watu ambao waliumizwa vibaya sana tangu Putin alipoanzisha uvamizi wake wa kila aina.

Soma pia: Biden: Nimechukizwa na shambulio la hospitali Gaza

 Rais huyo amema kuwa hawajashau makaburi ya umaa, miili iliyopatikana ikiwa na dalili za mateso, ubakaji uliotumiwa kama silaha na Warusi, na maelfu na maelfu ya watoto wa Ukraine waliotekwa nyara na kupelekwa Urusi na kuibiwa kutoka kwa wazazi wao.

Biden atarajiwa kutuma ombi la ufadhili wa dharura kwa bunge la Marekani

Biden amesema atatuma ombio la ufadhili wa dharura kwa bunge la nchi hiyo ambao unatarajiwa kuwa dola bilioni 105 kwa mwaka ujao. Ombi hilo litakalowasilishwa leo, linajumuisha dola bilioni 60 kwa Ukraine, zaidi zitakazotumiwa kuongeza akiba ya silaha za Marekani ambazo tayari zimetolewa.

Vikosi vya Israel Kusini vikishika doria Kusini mwa Israel karibu na ukanda wa Gaza mnamo Oktoba 18, 2023
Vikosi vya Israel Kusini vikishika doria Kusini mwa IsraelPicha: Jim Hollander/newscom/picture alliance

Biden ameongeza kuwa dola bilioni 14 ni za msaada kwa Israel na zingine bilioni 10 kwa msaada wa kibinadamu. Rais huyo amesema kuwa ufadhili huo ni uwekezaji bora ambao utakuwa na manufaa kwa usalama wa Marekani kwa vizazi vijavyo.

Upinzani waibuka katika bunge la seneti

Bunge la seneti linataka kuchukuwa hatua za haraka kuhusu pendekezo la Biden na kutumainia kuwa litaweka shinikizo kwa bunge hilo linalodhibitiwa na chama cha Republican kutatua mvutano wake wa uongozi na kurejelea shughuli zake. Hata hivyo, kuna upinzani katika bunge hilo kuhusu jinsi ya kusonga mbele. Wanachama wanane wa chama cha Republican, wakiongozwa na Seneta wa Kansas Roger Marshall, wanasema hawakutaka kuchanganya msaada kwa ajili ya Ukraine na Israel chini ya sheria sawa.

Soma pia:Biden kuomba fedha zaidi bungeni kwa ajili ya Israel na Ukraine

Kupitia barua walioandika, maseneta hao wamesema kuwa migogoro hiyo miwili ni tofauti na isiyohusiana na kwamba itakuwa makosa kuongeza msaada kwa Israel katika jaribio la hatimaye kuongeza msaada zaidi kwa Ukraine.

Hotuba ya Biden, inakuja siku moja baada ya ziara yake nchini Israel, ambapo alionesha mshikamano na taifa hilo katika mapigano yake na kundi la Hamas na kutoa shinikizo la msaada zaidi wa kibinadamu kwa Wapalestina walioko katika ukanda wa Gaza.

Soma pia: Biden aeleza wasiwasi kuhusu mgogoro wa kisiasa bungeni

Ikulu ya White House imesema kuwa kabla ya hotuba hiyo, Biden alizungumza na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy na kusisitiza kwamba Marekani bado imejitolea kuiunga mkono nchi hiyo.

Ofisi ya Oval ni mojawapo ya majukwaa yenye hadhi ambayo Rais anaweza kutumia kuelezea uzito wa hotuba yake wakati wa mgogoro.