1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin.Ujerumani kuondoa mabomu mtawanyiko duniani.

21 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8c

Ujerumani imezindua mpango wenye awamu tatu ili kuondoa kabisa mabomu mtawanyiko duniani.

Tangu wakati wa enzi za vita vya Vietnam , watu 100,000 wengi wao wakiwa raia , wameuwawa duniani kote na mabomu hayo.

Mengi yamelipuka muda mrefu baada ya kudondoshwa, na kuzuwia ujenzi mpya baada ya vita.

Muswada wa azimio uliotolewa na ofisi ya wizara ya mambo ya kigeni nchini Ujerumani utaweza katika awamu ya kwanza kuzuwia mara moja matumizi ya mabomu mtawanyiko duniani kote.

Hatimaye matumizi mbadala ya silaha hayatakuwa na madhara makubwa kwa raia. Ujerumani inasema kuwa majeshi yake yamepiga marufuku matumizi ya mabomu mtawanyiko mwaka jana.