1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Lengo ni kupunguza ukosefu mkubwa wa ajira

12 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEJ6

Viongozi wa vyama viwili vikuu nchini Ujerumani wametangaza maelezo ya makubaliano ya kuunda serikali ya muungano mkuu chini ya uongozi wa mhafidhina Bibi Angela Merkel.Alipozungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari,Kansela mteule Merkel alisema lengo kuu la makubaliano ni kupata nafasi zaidi za kazi nchini Ujerumani na kuchangamsha ukuaji wa kiuchumi.Siku ya Ijumaa,viongozi wa chama cha Social Demokrat na wahafidhina wa Christian Demokrat waliafikiana kuunda serikali ya mseto kufuatia majadiliano ya wiki nane.Juu ya hivyo,hati hiyo inahitaji kuidhinishwa katika mikutano maalum itakayofanywa na vyama vya CDU,CSU na SPD wiki ijayo.Baadae ndio mkuu wa chama cha CDU,Bibi Angela Merkel ataweza kuchaguliwa Novemba 22 kuwa Kansela wa kike wa kwanza nchini Ujerumani.Uchaguzi mkuu uliofanywa mwezi wa Septemba haukuweza kutoa mshindi dhahiri.