1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin: Polisi hawataki jeshi lisimamie usalama wakati wa Tamasha la Kombe la Dunia la Kabumbu mwakani hapa Ujerumani

12 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEvK

Chama cha maofisa wa polisi hapa Ujerumani kimeipinga fikra ya chama cha upinzani cha CDU hapa nchini kwamba jeshi litimiwe kulinda usalama, ikiwa ni pamoja na kufanya doria za kupambana na ugaidi, wakati wa michezo ya kombe la dunia la kandanda mwakani. Ujerumani itakuwa mwenyeji wa tamasha hilo. Msemaji wa chama cha maafisa wa polisi, Wolfgang Speck, amesema kutumiwa jeshi kutakuwa ni kinyume ya katiba ya Ujerumani. Alisema ni polisi peke yao ambao ni dhamana ya usalama wa umma ndani ya Ujerumani. Fikra hiyo pia imekataliwa na Chama cha kiliberali cha Free Democratic ambao huenda wakawa washirika wa Wa-Conservative katika serekali ijayo ya mseto.