1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Kansela wa Ujerumani kukutana na rais wa Ufaransa

7 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFYu

Kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder amemwalika rais wa Ufaransa Jacque Chirac nyumbani kwake hii leo,kwa mazungumzo ya kirafiki yatakayohusu masuala nyeti ya umoja wa Ulaya.

Viongozi hao wawili watazungumzia juu ya mkataba wa kudhibiti bajeti za nchi za Umoj wa Ulaya na suala la mcheketo wenye lengo la kuidhinisha katiba ya Umoja wa Ulaya.

Ujerumani na Ufaransa zimelaumu mkataba huo kwa kutokuwa na uwezo wa kubalidili malengo.

Kansela Schroeder na Jacque chirac ,wanatarajiwa hasa kuzungumzia hatua zinazoweza kuchukuliwa, dhidi ya nchi zao kwasababu ya kukiuka miongozo ya bajeti, inayowajibisha nchi za Umoja wa Ulaya kutovuka asilimia tatu ya pato jumla la taifa, katika nakisi za bajeti zao.