1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN-Idadi ya wasio na ajira yapungua kidogo nchini Ujerumani.

31 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFRb

Idadi ya watu wanaotafuta kazi nchini Ujerumani,ilishuka katika mwezi huu wa Machi,lakini bado idadi ya watu wasio na ajira inasimama palepale juu ya milioni tano.

Kwa mujibu wa takwimu zilizopatikana leo kutoka Idara ya Leba ya Shirikisho la Ujerumani,idadi ya watu wasio na ajira imepungua kwa mwezi huu wa Machi kwa watu 41,000.