1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLI-Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani atangaza mapendekezo ya kudhibiti ongezeko la wasio na ajira.

17 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFWA

Kansela wa Ujerumani Gerhard Schröder amewasilisha mikakati mipya yenye lengo la kupunguza kiwango cha juu cha watu wasio na ajira na hivyo kuamsha uchumi wa nchi.Katika hutuba yake bungeni leo,Kansela Schröder amesema mikakati hiyo inajumuisha vitegauchumi vyenye kugharimu euro bilioni mbili katika sekta ya usafiri na halikadhalika mageuzi zaidi katika upandee wa ajira.Pia amependekeza kufanywe marekebisho katika upande wa kodi kwa makampuni.Baadae leo Kansela Schröder atakutana na viongozi wa upande wa upinzani,Bibi Angela Merkel na Bwana Edmund Stoiber katika kikao kilichopewa jina la mkutano wa kilele wa kazi.Mkutano huo utajadili njia za kupambana na kupanda kiwango cha watu wasio na ajira hapa Ujerumani.

Zaidi ya watu milioni 5 na laki mbili hawana ajira nchini Ujerumani,kikiwa ni kiwango cha juu kabisa tangu kumalizika wa vita vikuu vya pili vya dunia.