1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Benki ya Dunia, Ufaransa kuikopesha Uganda dola milioni 600

6 Septemba 2024

Benki ya Dunia na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) zimetangaza kuipa Uganda mkopo wa zaidi ya dola milioni 600 kwa ajili ya miradi ya miundombinu na usimamizi wa taka jijini Kampala.

https://p.dw.com/p/4kM70
Jaa la takataka mjini Kampala
Jaa la takataka mjini KampalaPicha: Hajarah Nalwadda/XinHua/dpa/picture alliance

Taarifa hii imetolewa jana Alhamisi na serikali ya Uganda pamoja na Benki ya Dunia.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, dola milioni 566 ni mkopo kutoka Benki ya Dunia na dola milioni 42.7 zitatolewa na AFD.

Soma pia: Wanaharakati wanaopinga mradi wa mafuta Uganda wakamatwa

Mkopo huo umetolewa wakati raia wa Uganda wakilalamikia usimamizi wa takataka na barabara mbovu za mji mkuu, kutokana na bajeti ndogo kutoka serikalini.

Mwezi uliopita, maporomoko ya takataka yalifukia makaazi ya watu nje kidogo ya mji wa Kampala, na kusababisha vifo vya watu 35.