1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benki kuu ya dunia yaionya Kenya

Oumilkheir Hamidou
11 Oktoba 2018

Benki kuu ya dunia imeionya wizara ya fedha ya Kenya dhidi ya kupunguza bajeti za kusimamia miradi ya maendeleo.

https://p.dw.com/p/36LZ5
NO FLASH Weltbank in Washington
Picha: AP

Katika ripoti yake iliyotangazwa Jumanne tarehe 10.10.2018, Benki kuu ya dunia imeionya wizara ya fedha ya Kenya dhidi ya kupunguza bajeti za kusimamia miradi ya maendeleo kwa lengo la kupunguza mzigo wa madeni.

Katika tathmini yake inayotolewa mara mbili kwa mwaka, benki kuu ya dunia imesema kwa kufanya hivyo, nchi hiyo inaukaba ukuaji wa kiuchumi na kwa namna hiyo kupunguza mapato ya ndani.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, deni la Kenya linafikia asilimia 57 ya pato la ndani, kukiwa na upungufu wa sifuri nukta tano, ikilinganishwa na mwaka jana.

Ripoti hiyo inashauri serikali ya Kenya ipunguze badala yake bajeti ya mashirika yanayomilikiwa na serikali pamoja na viwango vya mishahara ya watumishi wa serikali.