1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benin yamkamata mkosaji mkubwa wa Rais Talon

21 Agosti 2024

Mkosoaji mkubwa wa mtandaoni wa Rais wa Benin Patrice Talon, amekamatwa kwa madai ya kuchapisha taarifa za uwongo na kuchochea uasi.

https://p.dw.com/p/4jj89
Benin | Kurudishwa kwa vitu vya sanaa huko Cotonou
Rais wa Benin Patrice Talon katika hafla ya kurejeshwa kwa vitu vya kale vilivyoporwa na wanajeshi wa Ufaransa wakati wa Ukoloni. Picha: Séraphin Zounyekpe

Vyanzo vya mahakama vimeeleza kuwa Steve Amoussou alikamatwa jana Jumanne na atafikishwa mahakamani baadae mwaka huu. Amoussou anafahamika sana nchini Benin kwa kumkosoa rais kwenye mitandao ya kijamii. Mwanablogu huyo, huwa anajiita ''mpinzani asiye na woga'', lakini sio mwanachama rasmi wa chama cha siasa. Amoussou, mwenye wafuasi 75,000 kwenye mtandao wa Facebook, amekuwa akiishi katika nchi Jirani ya Togo kwa miaka kadhaa. Wakili wake, Aboubakar Baparape, amesema mteja wake alikamatwa katika viunga vya mji mkuu wa Togo, Lome Agosti 12 na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi nchini Benin. Chama cha Wanasheria wa Benin, kimesema hatua hiyo ni ukiukaji wa wazi wa viwango vya sheria vya nchi hiyo, na kimetoa wito wa kuwepo uwazi.