1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bellingham avalia unahodha BVB

2 Oktoba 2022

Jude Bellingham amevalia unahodha katika kikosi cha Borussia Dortmund kwa mara ya kwanza siku ya Jumamosi lakini hakuweza kuzuia timu yake kushindwa na Cologne.

https://p.dw.com/p/4Hdya
Fussball Bundesliga | 1. FC Köln - Borussia Dortmund
Picha: Dennis Ewert/RHR-FOTO/picture alliance

Borussia Dortmund ilipoteza nafasi ya kukaa kileleni mwa ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga baada ya kupokea kipigo cha 3-2 kutoka FC Cologne.

Dortmund wameshindwa kuitumia fursa hiyo kabla ya mechi dhidi ya mabingwa watetezi Bayern Munich wiki ijayo.

soma Union Berlin waendelea kupaa kileleni mwa ligi

Kabla ya mchuano dhidi ya Cologne, kocha mkuu wa Borussia Dortmund Edin Terzic aliketi na Jude Bellingham kwa mazungumzo kwenye kona ya chumba cha kubadilishia nguo. Kutokana na kukosekana kwa nahodha wa klabu Marco Reus na naibu nahodha Mats Hummels ambaye anaugua, mkoba ulikabidhiwa kwa kijana huyo wa Uingereza, na ni rasmi atakuwa nahodha wa tatu katika kikosi cha BVB.

Baada ya Cologne kupata matokeo ya kuvutia katika kipindi cha pili na kushinda 3-2, Bellingham aliwaongoza wachezaji wenzake hadi kwa mashabiki, akiwa ameenua mikono ishara ya kukubali kuwajibika.

"Je, yeye ndiye nahodha mdogo zaidi katika historia ya Borussia Dortmund?" aliuliza Terzic mwenyewe katika mahojiano kabla ya mechi. "Hatujui. Lakini kwa hakika ana umri wa kutosha."

Bellingham: "Ndoto imetimia"

Fussball Bundesliga | 1. FC Köln - Borussia Dortmund
Picha: Martin Meissner/AP/picture alliance

Kipaji vya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 katika chenga, kutoa pasi, utulivu na nidhamu ya ulinzi vimekuwa wazi kwa muda, na uwezo wake wa kubadilisha hali ya ulinzi kuwa ya ushambuliaji mara nyingi umeisaidia Dortmund kutoka katika mazingira magumu kimchezo.

"Wakati niliposajiliwa kwa klabu hii mara ya kwanza, sikuwahi kufikiria kuwa ingewezekana," alikiambia kituo cha Bundesliga. "Lakini baadaye nilikutana na wachezaji na walinipa imani kwamba siku moja naweza kuwa nahodha."

Sevilla na Bayern 

Fussball Bundesliga | 1. FC Köln - Borussia Dortmund
Picha: Dennis Ewert/RHR-FOTO/picture alliance

Maafisa wa Dortmund wana matumaini kwamba naibu nahodha Hummels, ambaye alikosa mechi dhidi ya Cologne kwa sababu ya homa kali, atapatikana tena kwa mechi dhidi ya Sevilla kwenye Ligi ya Mabingwa siku ya Jumatano na pia katika mechi ya Jumamosi ijayo dhidi ya mabingwa watetezi Bayern Munich.

 

https://p.dw.com/p/4Hdgp