1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT:Katibu Mkuu Annan atembelea jeshi la kulinda amani kusini mwa Lebanon

29 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDH4

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa bwana Kofi Annan leo amelitembelea jeshi la Umoja huo linalolinda amani kusini mwa Lebanon.

Bwana Annan pia amezitembelea sehemu kadhaa za Lebanon ili kujijuvya kiwango cha maangamizi yaliyoikumba nchi hiyo kutokana na vita vya wiki nne baina ya majeshi ya Israel na wapiganaji wa Hezbollah.

Bwana Annan anatazamiwa kuwasili Isreal leo ambapo atakuwa na mazungumzo na viongozi wa chi hiyo juu ya hatua za kijeshi ambazo Israel bado inatekeleza dhidi ya Lebanon.

Majeshi ya Israel bado yemezifunga bandari na viwanja vya ndege vya Lebanon.