1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing. Kiongozi wa Palestina yuko ziarani China.

17 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFCZ

Kiongozi wa Palestina Bwana Mahmoud Abbas amewasili mjini Beijing leo kwa ziara yake ya kwanza nchini China tangu kuchukua madaraka hayo, huku kukiwa na matumaini kuwa atataka kuungwa zaidi mkono na taifa hilo lenye nguvu katika bara la Asia.

Kwa mujibu wa ubalozi wa Palestina mjini Beijing , Bwana Abbas ambaye atakuwa nchini China kwa muda wa siku mbili, anatarajiwa kukutana kesho la rais Hu Jintao na waziri mkuu Wen Jiabao .

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni Kong Quan amewaambia waandishi wa habari kuwa Bwana Abbas ataifahamisha China kuhusiana na maendeleo ya hivi karibuni katika mashariki ya kati.

Amesema pia kuwa pande hizo mbili zitazungumzia kuhusu ushirikiano wenye manufaa kwao, na kutia saini makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi.

China ilianzisha uhusiano wa kibalozi na Palestina katika mwaka 1988.

Bwana Abbas amewasili China akitokea Japan ambako alipata ahadi ya kupatiwa dola milioni 100 za amsaada kwa mamlaka ya Palestina.