BEIJING: Ban Ki Moon ziarani China
27 Oktoba 2006Matangazo
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Korea Kusini, Ban Ki Moon, atakayechukuwa wadhfa wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka ujao, amewasili China kujadili mzozo wa mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.
Ziara hiyo ni sehemu ya ziara yake ya mataifa matano wanachama wa kudumu katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Ban Ki Moon anatarajiwa kukutana na rais wa China Hu Jintao, kansela Tang Jiaxuan na waziri wa mambo ya kigeni Li Zhaoxing.
China na Korea Kusini, majirani wa karibu wa Korea Kaskazini, zimeunga mkono vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini kwa kufanya jaribio la zana zake za kinyuklia mnamo Oktoba 9.
Lakini China imeeleza wasiwasi wake kwamba kuishinikiza sana Korea Kaskazini huenda kusababishe hali ya wasiwasi katika eneo hilo.