1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern watoa keki kwa wazee na watumishi

Josephat Charo
1 Mei 2020

Tukio hilo la ukarimu linanuiwa kuwatia moyo vikongwe na kuwahakikishia kwamba jamii iko pamoja nao wakati huu wa janga la corona.

https://p.dw.com/p/3bfjR
Vorstandsvorsitzender Karl-Heinz Rummenigge, FC Bayern München
Picha: picture-alliance

Mabingwa watetezi wa ligi ya Bundesliga Bayern Munich wanatoa keki kwa nyumba 80 za kuwaangalia wazee katika jimbo la Bavaria kama hatua ya kuonesha huruma na mshikamano na wazee na watumishi wakati wa janga la virusi vya corona.

Bayern imesema katika taarifa siku ya Ijumaa (01.05.2020) kwamba kwa kushirikiana na wizara ya afya ya jimbo la Bavaria 10 kati ya keki maarufu kwa jina Sachertorten zitakwenda kwa kila nyumba ya wazee wiki ijayo.

"Wazee ndio watu wanaoteseka zaidi kutokana na corona, kisaikolojia pia. Safari za kuwatembelea haziruhusiwi. Tunataka kuwaambia kwa kutumia ukarimu huu: hamko peke yenu," alisema mwenyekiti wa klabu ya Bayern, Karl-Heinz Rummenigge.

"Watumishi wa wazee hufanikisha mambo makubwa kwa jamii kila siku.Kazi hii inahitaji nguvu nyingi na kujitolea sana. Lazima wawe na sifa nyingi kitaaluma na hata huruma," aliongeza kusema.

Ligi ya Bundesliga ilisitishwa katikati ya mwezi Machi kwa sababu ya janga la virusi vya corona. Vilabu vina matumaini ya kuukamilisha msimu kuanzia mwezi Mei kuendelea.

(dpae)