1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAYERN MUNICH YAONGOZA BUNDESLIGA KWA POINT 6:RAIS WA FIFA AKAMILISHA ZIARA YAKE AFRIKA

18 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CHZE

BUNDESLIGA

Bayern Munich yaelekea itatawazwa tena mabingwa wa Ujerumani. Siku tatu tu baaada ya kutimuliwa nje ya Kombe la klabu bingwa barani Ulaya na Chelsea ya Uingereza,imefungua mwanya wa point 3 kati yake na Schalke 04.

Owen Hargreaves aliipatia Bayern munich bao dakika ya mwisho hapo jumamosi katika mpambano na Hannover na kuipatia pointi 3.

Schalke iliokua hadi mwishoni mwa juma lililopita pointi sawa na Bayern Munich,ilipoteza pointi 3 katika changamoto na Hamburg iliomalizika 2:1.Timu nyengine iliokua nafasi ya tatu Stuttgart ilizabwa mabao 2:1 na Rostock.Mechi 5 tu zikisalia kabla msimu kumalizika, Bayern Munich inaongoza ngazi ya Ligi kwa point 62 ikifuatwa nyuma na Schalke yenye pointi 56.

Nuremberg imenyakua jana pointi 3 na kujikomboa kutoka safu ya kuteremka daraja ya chini ilipoitoa Wolfsburg kwa bao 1:0

Msenegal Mamadou Diabang alitia bao muhimu la ushindi kwa Bochum dhidi ya Kaiserslauten na kukaribia nayo kuikomboa nje ya safu ya kuzama daraja ya pili.

Katika dimba la Afrika:

APR FC ya Rwanda imepigwa kumbo nje ya Kombe la shirikisho la dimba la Afrika kwa kushindwa kuandaa nyumbani duru yao ya tatu ya Kombe hilo na Ismailia ya Misri mwishoni mwa wiki iliopita.Hii ni kwa muujibu wa wakuu wa CAF.

Wamisri walizuwiliwa kuingia Rwanda kwa mpambano huo wa April 10 kutokana na maombolezi ya wiki nzima ya mauaji ya halaiki yaliotokea 1994.

Ismailia iliarifiwa juu ya kuahirishwa kwa mpambano huo walipokua njiani wakibadili ndege mjini nairobi kutaka kuelekea Kigali.

CAF imesema Warwanda walishindwa kuwaarifu wenzao wamisri na mapema ombi lao la kutaka kuahirisha mchezo huo.

Serikalio ya rwanda ilipiga marufuku kalenda nzima ya michezo katika kipindi hicho cha maombolezi.

Ismailia sasa itacheza na timu itakayoshindwa katika mpambano wa Kom,be la klabu bingwa kati ya Esperence ya Tunisia na Kaizer Chief ya Afrika Kusini mwezi ujao.

Tukisalia Kigali: Rais wa FIFA Sepp Blatter alikamilisha mwishoni mwa wiki ziara yake ya siku 6 katika Afrika magharibi na Kati baada ya kuanzisha miradi ya maendeleo ya soka inayogharimiwa na FIFA-shirikisho la dimba ulimwenguni katika nchi hizo 5 alizozitembelea:Chad,Jamhuri ya afrika ya Kati,Kongo-Kinshasa,Burundi na mwishoe Rwanda.

Blatter alaikuwa pia na hamu ya kuimarisha mahusiano na kundi la nchi hizi ambazo hazikumpigia kura ama 1998 au 2002.

Afrika ni bara la kwanza kabisa kunufaika na mradi wa maendeleo ya FIFA-maarufu ‘MRADI GOAL" ulioasisiwa 1999 kwa kima cha faranga milioni 100 za kiswisi kwa muda wa miaka 3 na ukarefushwa kwa miaka 3 mengine hapo 2003 kwa kima hicho hicho cha faranga milioni 1000 sawa na dala milioni 83.3.

Timu ya Taifa ya Zanzibar ilipangwa kucheza leo na ile ya Zimbabwe mjini Harare sehemu ya sherehe za uhuru wa Zimbabwe.Hadi adhuhuri leo,timu hiyo ilikuwa uwanja wa ndege wa zanzibar ikisubiri ndege kuichukua kutoka Zimbabwe.Timu ya zanzibar ilikua iondoke jana .

Bingwa wa zamani wa dunia wa nusu-marathon, Martin Lel kutoka Kenya, ndie aliewika jana na kushinda mbio za London marathon akimpiku bingwa wa rekodi ya dunia Paul Tergat. Bingwa wa dunia Mmorocco Jaouad Gharib alikuja wapili.Evans Rutto akamaliza 3 Rutto . Paul Tergat alieweka mjini berlin rekodi ya dunia miaka 2 iliopita na hakuwahi kushinda London marathon,alibnidi kuridhika na nafasi ya 8.