1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern Munich kutwaa taji la Bundesliga wikiendi hii?

11 Juni 2020

Klabu ya soka ya Bayern Munich inatarajia kujihakikishia kulitwaa taji la ligi kuu ya kandanda ya Bundesliga msimu huu, pale itakapopambana uso kwa uso na Borussia Moenchengladbach.

https://p.dw.com/p/3ddRD
DFB Pokal Bayern vs Frankfurt Jubel Bayern 2:1
Picha: Reuters/K. Pfaffenbach

Endapo Buyern Munich itafanikiwa kulitwaa taji la Bundesliga msimu huu, hii itakuwa ni mara ya nane mfululizo kwa timu hiyo kulitwaa kombe la ligi hiyo, ambalo ligi yake hivi sasa inachezwa bila ya kuwa na mashabiki uwanjani kufuatia mripuko wa virusi vya Corona.

Kwa hivi sasa timu ya Bayern Munich inaongoza kwa kuwa kileleni mwa ligi hiyo ya Bundesliga ikiwa na alama 67 ikiwaacha wapinzani wao Borussia Dortmund wanaoshikilia nafasi ya pili kwa kuwa na alama 63.

Bayern, itajihakikishia taji hilo katika michezo mitatu iliyosalia endapo kama itashinda, na timu inayoshikilia nafasi ya tatu kutoka mkiani, Fortuna Dusseldorf iifunge Borussia Dortmund inayoshikilia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo.

Mechi ya Fortuna Dusseldorf na Borussia Dortmund itakamilika saa moja kabla ya kuanza kwa mechi ya Bayern Munich dhidi ya Borussia Monchengladbach siku ya Jumamosi (13.06.2020.) Na endapo Dortimund ikipoteza mchezo wake dhidi ya Dusseldorf, hiyo itakuwa ni nafuu kwa Bayern Munich.

Bayern inateremka uwanjani wikiendi hii huku ikiwakosa nyota wake kadhaa akiwemo Robert Lewandowski na Thomas Mueller ambao wote kwa pamoja walifungiwa kucheza baada ya kuonyeshwa Kadi mbili za njano katika mechi iliyopita ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Bayer Leverkusen.