1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Historia

Bayajida - baba wa kabila la Hausa

25 Julai 2018

Bayajida anaonekana kama baba wa watu wa kabila la Hausa. Na kwa mujibu wa maelezo ya utamaduni na jadi katika eneo hilo, alikuwa ni Mwarabu aliyeunda maskani yake kaskazini mwa Nigeria.

https://p.dw.com/p/2rJS0

Wanahistoria  wanashaka kwamba  Bayajida  alikuwa  kiumbe  wa  kweli, lakini  hekaya  za Bayajida  bado  ni imara. Zinamweleza  kama  mtu  ambaye ukoo wake ndio ulioasisi  taifa  la Hausa. Mabadiliko  muhimu katika  jamii  yanahusishwa  na  yeye, na  hekaya  hizo zinaadhimishwa  kila  mwaka  mjini Daura, nchini  Nigeria.

Ni wakati gani Bayajida aliishi? 

Sehemu  kubwa  ya  hekaya  za Bayajida  ilielezewa  kupitia  historia ya  mazungumzo. Hakuna rekodi  ya  tarehe  aliyozaliwa  Bayajida  ama   kifo  chake, na  hakuna  uhakika  wa  kuwapo  kwake. Anaaminika  kuwa  alitokea  Baghdad  katika  nchi  ya  sasa  ya  Iraq, na baada  ya  kukutana  kwa  muda  na  himaya  ya  Kenem  mjini  Bornu, aliweka  makaazi  yake  Daura,  ambao  sasa  ni Katsina.

Bayajida: Hekaya za taifa la Hausa

Lakini  nini  hasa  chanzo  cha  hekaya  hii? 

Baadhi  ya  vyanzo vinaeleza  kwamba  hekaya  za Bayajida zinaonekana  mahali fulani  kati  ya  karne  ya  16 na 19, wakati  tayari  kulikuwa na  ushahidi  wa  kuishi kwake  katika  utamaduni  wa  Wahausa kati  ya  karne  ya  9  na 10.

Nini  maana  ya  jina  lake?

Jina  lake  la  asili  huenda  lilikuwa Abu Zaid. Jina  hilo  alilopewa  na  wahausa, Bayajida , kwa  hakika  ni  neno: "Ba ya ji da" , likiwa  na  maana "aliyekuwa  kwanza  haelewi".

Nilisikia kuhusu mvuto kwa nyota hadithi inasemaje ? 

Bayajida anasemekana  kwamba  alimuuwa  nyoka  ambaye  aliishi  kisimani kijijini Kusugu, sehemu  ambayo ni  Daura  ya  sasa. Nyoka huyo  alikuwa  akiwasumbua  watu  na  kuwazuwia  kuteka  maji, nyoka  huyo  aliruhusu  watu  kuchota  maji  kutoka  katika  kisima  hicho siku  ya  Ijumaa  tu. Mbali na tahadhari  zilizotolewa  kwake, Bayajida alikwenda  kuchota  maji  katika  kisima  hicho siku  ya  Alhamis. Wakati  nyoka alipomshambulia, Bayajida alikwenda  kuchota  maji katika  kisima  hicho  siku  ya  Alhamis. Nyota  alipomshambulia , alimkata  kichwa  chake kwa  upanga.

Hadithi yake ina mwisho mzuri?

kama  zawadi  ya  kumuua  nyoka, malkia  wa Daura,  Daurama aliahidi  kumpa  nusu  ya  ufalme wake . Lakini  Bayajida kwa  werevu  alikataa  na  badala  yake  alimuomba malkia  amuoe. Hii  ilikuwa  haijawahi  kutokea, kwa  kuwa malkia  wote  hubaki  bila  kuolewa  maisha  yake  yote. Hata  hivyo , Daurama  alikubali  kwa  kuwa  alijihisi ana  deni  kwake.

DW African Roots- Bayajida
Picha: Comic Republic

Nini  alichokiacha: 

Bayajida  anajulikana kwa  kubadilisha  utamaduni  katika  ufalme  wa daura: Kabla  ya  kuwasili, katika ufalme  wa  Daura  ulikuwa  unatawaliwa  tu  na  wanawake. Utamaduni  ulibadilika  kutoka  utawala  wa  wanawake hadi  utawala  wa  wanaume  baada  ya  kumoa  malkia daurama  na  watoto  wake  wa  kiume  walirithi utawala  wake.

Taifa  la Hausa:

Bayajida  alipata  watoto  watatu  wa  kiume:  mke wake  wa  kwanza (mtoto wa  mtawala  wa  ufalme  wa Borno) alimuita Biram, mmoja  wa  malkia Daurama, aliyeitwa  Bawo, na  mmoja  wa  mahawara. Bawo alipata  watoto  sita  wa  kiume, ambao , pamoja  na  mjomba  wao Biram, walikuja  kuwa  watawala  majimbo  halali  saba  ya  Hausa  ambayo  yanafahamika  kufuata : Daura, Kano, Katsina, Zaria, Gobir, rano na  Hadeja.

Mwandishi: Sekione Kitojo

Mhariri: Yusuf Saumu 

Pinado Abdu-Waba, Abdoulaye Mamman Amadou na Gwendolin Hilse wamechangia kuandika makala hii. Ni sehemu ya makala maalum za  mfululizo wa "Asili ya Afrika", ushirikiano kati ya shirika la DW na taasisi ya Gerda Henkel.