1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Barua pepe yasema Annan alikua na taarifa.

15 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF3S

Umoja wa mataifa /New York.

Kumegunduliwa barua pepe inayoashiria kupingana na madai ya Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan ya kutohusika na kandarasi aliyopewa mwajiri wa zamani wa mwanawe wa kiume Kodjo Annan, kuhusika na mpango wa mafuta kwa ajili ya chakula nchini Iraq. Barua hiyo pepe au email inaeleza kwamba 1998 kulifanyika mkutano mjini Paris kati ya Bw Annan na Wakuu wa kampuni ya ukagusi ya COTECNA, ambapo aliwaahidi uungaji mkono wa Umoja wa mataifa. Wiki chache baadae kampuni hiyo yenye makao yake makuu mjini Geneva-Uswisi ikapewa kandarasi ya kuukagua mpango huo wa mafuta kwa chakula nchini Iraq. Barua hiyo pepe inaeleza kwamba , mwanawe Bw Annan , Kodjo alikua ni mshauri wa kampuni hiyo ya COTECNA, wakati mkutano huo ulipofanyika. Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa amekanusha kuwa na taarifa yoyote juu ya makubaliano hayo. Msemaji wa Umoja wa mataifa Fred Eckhard amesema Bw Annan pia hana kumbukumbu yoyote kuhusu mkutano huo wa Paris.