1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la usalama kujadili vikwazo dhidi ya Gaddafi

26 Februari 2011

Wakaazi wa Tripoli wanajiandaa kukabiliana na mapambano makali baada ya Gaddafi kuwaambia wafuasi wake atawapa silaha waitetee Libya

https://p.dw.com/p/10Q2n

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linakutana tena leo kujadili azimio la kumuwekea vikwazo kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi, katika juhudi ya kukomesha ukandamizaji wa umwagaji damu dhidi ya waandamanaji nchini Libya. Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Marekani zimetayarisha azimio linalosema mashambulio dhidi ya raia huenda yakafikia kiwango cha kuitwa uhalifu dhidi ubinadamu. Azimio hilo pia linataka Libya iwekewe kikwazo cha silaha, marufuku ya kusafiri na kuzuiliwa kwa mali za Gaddafi na wapambe wake.

Mkutano wa leo unafanyika siku moja baada ya balozi wa Libya katika Umoja wa Mataifa, Mohammed Shalgham, kulitolea mwito Baraza la Usalama la umoja huo kuchukua hatua za haraka kuwalazimisha viongozi wa Libya wakomeshe ukandamizaji wa umwagaji damu dhidi ya waandamanaji. Shalgham amesema ukatili dhidi ya raia nchini Libya lazima ukome mara moja.