1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bao la sekunde ya mwisho lawaokoa Barcelona

14 Februari 2022

Goli la dakika ya mwisho la mchezaji Luuk de Jong liliwapelekea Barcelona kupata sare ya magoli 2 dhidi ya mahasimu wao wa Catalunya, Espanyol katika Dabi Barceloni kwenye Ligi Kuu ya Uhispania La Liga hapo Jumapili.

https://p.dw.com/p/470Bd
Fußball Katar | Trainer Al Sadd SC Xavi Hernandez
Picha: Nikku/XinHua/picture alliance

Barcelona ndio walioingia uongozini ila Espanyol walisawazisha na kuongeza goli la pili kabla miamba hao hawajasawazisha.

Sare hiyo inawapelekea Barca kuruka hadi katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa La Liga wakiwa na pointi 39 sawa na Atletico Madrid wanaoishikilia nafasi ya tano katika mbio za kuwania nafasi ya kushiriki Ligi ya Vilabu Bingwa Ulaya msimu ujao.

Kocha wa Barcelona Xavi Hernandez anasema ingawa alitaka ushindi, sare si matokeo mabaya kama kupoteza mechi kabisa.

"Si pigo kubwa mno kwa kuwa tumepata pointi moja, huu ni uwanja ambao si rahisi kupata matokeo ukizingatia kwamba vinara wa ligi Real Madrid walipoteza mechi yao hapa, mashabiki wao wanaipenda na kuishabikia timu yao kwa dhati. Nafikiri tulicheza vyema ila hatukutumia nafasi zetu na tulipofanya makosa ndipo walipotuadhibu," alisema Xavi.

Kibarua kinachofuata kwa Barcelona sasa ni katika Europa League siku ya Alhamis.