1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Banjul. Rais Jammeh ashinda uchaguzi.

24 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD9c

Nchini Gambia rais wa sasa Yahya Jammeh ameshinda uchaguzi wa rais nchini humo. Jammeh ,ambaye aliingia madarakani kwa njia ya mapindizi miaka 12 iliyopita , ameshinda asimilia 67 ya kura.

Hasimu yake mkubwa , mwanasheria anayetetea haki za binadamu Ousainou Darboe amepata asilimia 27.

Maafisa wa uchaguzi wamesema kuwa kumekuwa na tatizo la watu wachache kujitokeza ikiwa watu 400,000 tu ndio waliojitokeza kupiga kura.

Jumuiya ya kiuchumi ya Afrika magharibi ECOWAS yenye wanachama 15 ambayo imetuma wachunguzi wake katika uchaguzi huo, imesema kuwa uchaguzi ulifanyika katika hali ya uwazi na yenye kuaminika.