1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BANJUL: Rais Jammeh aongoza nchini Gambia

23 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD9q
Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi wa rais uliofanywa nchini Gambia siku ya Ijumaa yanaonyesha kuwa rais wa hivi sasa Yahya Jammeh anaongoza kwa asili mia 70 baada ya kura kuhesabiwa katika majimbo 22 ya uchaguzi kutoka jumla ya 48. Mpinzani wake mkuu,mwanasheria anaegombea haki za binadamu,Ousainou Darboe amejikingia asili mia 25 ya kura hizo.Mwana sosiolojia Halifa Sallah amepata kama asili mia 5 ya kura zilizohesabiwa. Rais Jammeh,alijinyakulia madaraka katika mapinduzi ya mwaka 1994 bila ya kumuaga damu.