1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Bangladesh kuunda serikali mpya ya mpito

8 Agosti 2024

Bangladesh inatazamia kupata serikali mpya ya mpito hivi leo itakayoongozwa na mchumi na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Muhammad Yunus.

https://p.dw.com/p/4jDpF
Muhammad Yunus, kiongozi mteule wa serikali ya mpito ya Bangladesh.
Muhammad Yunus, kiongozi mteule wa serikali ya mpito ya Bangladesh.Picha: Raphael Lafargue/abaca/picture alliance

Serikali hiyo iliyopewa jina la "serikali ya washauri" inatazamiwa kuapishwa wakati wowote kuanzia sasa.

Yunus, mwenye umri wa miaka 84, amependekezwa kuchukuwa nafasi hiyo na wanafunzi wenyewe, walioongoza vuguvugu la kumpinduwa Hasina.

Soma zaidi: Rais wa mpito wa Bangladesh kuapishwa Alhamis

Mchumi huyo ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa Hasina, anatazamiwa kuwasili mjini Dhaka akitokea Paris alikokuwa kwenye matibabu.

Licha ya umri wake mkubwa, viongozi wa wanafunzi na makundi mengine ya wanaharakati wanaamini kuwa ndiye mtu anayefaa kuiongoza Bangladesh kuelekea uchaguzi mkuu, na kuondosha uwezekano wa taifa hilo la kusini mwa Asia kuangukia mikononi mwa jeshi.