1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Katibu Mkuu Annan ziarani Iraq

12 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEJI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amekwenda Iraq kwa ziara ya ghafla.Hii ni ziara yake ya kwanza nchini humo tangu vikosi vilivyoongozwa na Marekani,kuiangusha serikali ya Saddam Hussein mwaka 2003.Ziara ya Annan inafanywa siku moja baada ya waziri wa kigeni wa Marekani,Bibi Condoleezza Rice pia kuizuru Iraq kwa ghafula.