1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. PKK kudhibitiwa zaidi.

31 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ax

Maafisa wa Iraq wamesema kuwa wanaongeza juhudi za kuwadhibiti waasi wa Kikurd wa PKK kufanya shughuli zao nchini na pia kuweza kupata kuachiliwa huru kwa wanajeshi wanane wa Uturuki wanaoshikiliwa na

kundi hilo lililoko kaskazini mwa Iraq. Waziri wa mambo ya kigeni Hoshiyar Zebari amesema nchi yake pia haijakata tamaa ya kufikiwa kwa suluhisho la mzozo na Uturuki. Zebari ametoa matamshi hayo baada ya kukutana na mwenzake wa Iran Manouchehr Mottaki ambaye alikuwa katika mji mkuu wa Iraq kuzungumzia juu ya suala la PKK. Uturuki imeongeza mbinyo dhidi ya Iraq kuchukua hatua dhidi ya wapiganaji, wanaokadiriwa kufikia 3,000 katika maeneo ya mlimani ya kaskazini mwa Iraq.

Kutokea huko , Uturuki inadai , wapiganaji hao wanafanya mashambulizi katika maeneo ya kusini mashariki ya Uturuki.