1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zoezi la uchaguzi Gabon laanza kwa kuchelewa

26 Agosti 2023

Zoezi la kupiga kura lilichelewa kuanza katika baadhi ya maeneo nchini Gabon hii leo, wakati raia wa taifa hilo wakimiminika vituoni kushiriki uchaguzi wa rais, bunge na serikali za mitaa.

https://p.dw.com/p/4VbvN

 

Uchaguzi ulitarajiwa kuanza saa moja asubuhi lakini baadhi ya vituo vya kupigia kura vilifunguliwa kwa kuchelewa na vingine havikufunguliwa kabisa. Sababu ya kucheleweshwa huko bado haijajulikana na tume ya uchaguzi haijatoa tamko kuhusiana na hilo.

Upinzani unatarajia kuchukua ushindi katika uchaguzi huu na kuyafuta matumaini ya Rais anaetetea kiti chake Ali Bongo, kuiongoza nchi hiyo kwa muhula mwengine wa tatu na kumaliza pia utawala wa familia yake iliyoitawala nchi hiyo kwa miaka 56.

Jumla ya wagombea 18 wanashiriki katika uchaguzi wa leo, sita kutoka vyama vikuu ya upinzani wamemuunga mkono mgombea mmoja.