1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Azimio nambari 1701 linaheshimiwa anasema Kofi Annan

13 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDCj

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan amesifu juhudi za kutia njiani azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa la kumaliza vita vya Libnan.Katika taarifa yake iliyotangazwa mjini New-York,katibu mkuu wa umoja wa mataifa amesema makubaliano ya kuweka chini silaha kati ya Israel na wanamgambo wa Hisbollah yanaheshimiwa.Israel imeshaihama thuluthi mbili ya eneo ililolikalia wakati wa vita. Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan anasisitiza umuhimu wa kupokonywa silaha wanamgambo wa Hisbollah ili kuepukana na balaa la kuzuka upya mzozo wa kijeshi.