1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AUFHAUSEN:Mabaki ya mtu wa kale yagunduliwa Bavaria,Ujerumani.

30 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEfz

Wanasayansi wa mambo ya kale,wamesema leo kuwa wamegundua mabaki ya mifupa ya mwanadamu mwanamke aliyeishi miaka 7,300 iliyopita,enzi za matumizi ya mawe ama stone age,Bavaria nchini Ujerumani.

Ugunduzi wa namna hiyo ni adimu sana kwa eneo la Bavaria na mwanamke huyo inaaminika alitoka katika jamii ya kundi la kwanza kabisa la wakulima waliofanya makazi yao maeneo ya kusini mwa Ujerumani.

Mapema mwaka huu wanasayansi hao mambo ya kale,waligundua mabaki ya mifupa ya mwanadamu aliyeishi miaka 5,300 kabla ya Kristo,maeneo ya mashariki mwa Ujerumani katika mji wa Leipzig,wakati walipokuwa wakichimbua makazi ya zamani pamoja na makaburi karibu na uwanja wa ndege.