1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Armenia na Azerbaijan zashambuliana

13 Mei 2023

Wanajeshi wa Armenia an Azerbaijan wameshambuliana kwa bunduki na silaha nyingine ikiwemo mabomu ya umbali mfupi saa chache kabla ya mazungumzo ya kutafuta mkataba wa amani ya kudumu baina ya mataifa hayo mawili.

https://p.dw.com/p/4RIaT
ARCHIV | Konflikt Aserbaidschan Armenien | armenische Soldaten
Picha: ARIS MESSINIS/AFP

Inaarifiwa mapigano hayo yamesabababisha kila upande kupoteza askari wake mmoja. Uhasama huo unashuhudiwa kuelekea mkutano uliopangwa siku ya Jumapili mjini Brussels kati ya waziri mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan na rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan. Mkutano huo unalenga kutafuta suluhu ya kudumu ya mvutano wa muda mrefu kati ya mataifa hayo juu ya eneo la Nagorno -Karabakh.

Kwa miongo mitatu mataifa hayo yaliyokuwa sehemu ya Dola ya Kisovieti yanapigana kuwania eneo hilo lenye wakaazi wengi wenye asili ya Armenia lakini linatambulika kama sehemu ya Azerbaijan.