1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ARGENTINA NI MABINGWA KOMBE LA VIJANA LA DUNIA-OLIMPIK 2012 YAAMULIWA WIKI HII

4 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CHYz

Visa vya mastadi 2 wa Brazil-mmoja anaeichezea Bundesliga na mwengine anaetaka kuiacha mkono Santos kujiunga na Real Madrid:

Robinho mshambulizi wa miaka 21 wa klabu ya Santos, mara mbili hakuhudhuria mazowezi ya klabu yake tangu kurudi Ujerumani alikoibuka bingwa na Brazil katika Confederations Cup.Robinho aliwaaga mashabiki wa Santos mara tu Brazil ilipoikomea Argentina mabao 4:1 na kutwaa Kombe hilo la mashirikisho.

Rais wa Santos ,Marcelo Teixeira,haraka alimkumbusha Robinho kwamba ana mkataba na santos hadi 2008 na kwamba klabu coyote inayomtaka Robinho itapaswa kulipa kitita cha dala milioni 50.eala Madrid ambako anafunza kocha wa zamani wa Brazil Luxemburgo ,anaemjua vyema Robinho, imejitolea kitita cha dala milioni 30 kwa chipikizi huyo.

Bundesliga ikiwa likizoni hadi mwezi ujao,stadi wa Brazil anaeichezea Hertha Berlin, Marcelinho anaripotiwa alipigana katika kilabu cha starehe kwao Brazil mwezi uliopita-gazeti la Ujerumani BILD liliripoti jana.Marcelinho mwenye umri wa miaka 30,amichezea Brazil mara 5 na anasemekana alipigana na mwanafunzi Jackson Alves de Azvedo ambae anaeripotiwa alizimia na kuumizwa meno.

Marcelinho aliechaguliwa mchezaji bora kabisa wa dimba msimu uliopita wa Bundesliga, na gazeti la dimba Kicker, amekanusha na kusema hana hatia yoyote. Meneja wa klabu yake ya Berlin,Dieter Hoeness anamuamini aliyosema.

KOMBE LA DUNIA LA VIJANA LAENDA ARGENTINA:

Argentina ilitawazwa jumamosi mabingwa wa Kombe la dunia la vijana chini ya umri wa miaka 21 baada ya kuiadhibu Nigeria kwa mabao 2:1 ya mikwaju ya penalty.

Argentina ilitia bao la kwanza la penalty ,lakini katika kipindi cha pili,Nigeria ilisawazisha kwa bao maridadi kabisa la kichwa alilotia Ogbuke.Mlinzi wa Nigeria,akafanya madhambi mengine na kinyume na mondo wa mchezo,Lionel Messi akaufumania tena kwa mara ya pili mango wa Nigeria kwa bao lake la 2 la penalty.

Nigeria, ikapoteza Kombe ambalo kwa kweli,lilikuwa lao.Mabingwa watetezi Brazil,waliolazwa katika nusu-finali na Argentina,walimaliza nafasi ya tatu nyuma ya Nigeria.

Brani Afrika,polisi waliingialia kati kurejesha utulivu pale wachezaji wa timu 2 za Tunesia-Etoile du sahel na Esperente walipopambana uwanjani na mwishoe kutoka suluhu 0:0 katika kinyan’ganyiro cha Kombe la klabu bingwa barani Afrika.Machafuko yalizuka mnamo dakika ya 80 ya mchezo pale wachezaji wa timu hizo mbili walipoanza kupigana ngumi.Hii ilifuatia mlinzi wa Etoile, Seif Ghezal kuangushwa chini baada ya kusukumwa na Marcos Pereira wa Esperence.Polisi wakaingia uwanjani kuwatenganisha wachezaji.

Esperence sasa ina miadi jumamosi ijayo na ASEC Abidjan ya Ivory Coast mjini Tunis wakati mahasimu wao Etoile wanakumbana na mabingwa mara 5 Zamalek jumapili mjini Cairo.

Stadi wa simba wa nyika-Kamerun, Salomon Olembe ameazimwa na klabu yake ya Marseille kwa Real Mallorca ya Spain.Mallorca wakitaka waweza pia kumnunua Olembe ambae msimu wa mwaka 2003/04 aliazimwa kuichezea Leeds United ya Uingereza.

Katika mbio za motokaa,bingwa mara 7 wa dunia,Michael Schumacher wa Ujerumani alisema hangeweza kufanya bora kuliko nafasi ya tatu aliomalizia jana katika mbio za Grand Prix nchini Ufaransa.Schumacher ambae msimu huu umemuendea kombo, alimaliza sek. 22 nyuma ya bingwa Fernando Alonso kutoka Spain.

Katika mashindano ya ubingwa wa tennis ya wimbeldon,Uingereza, Roger Federer alijipatia jana ushindi wake wa tatu mfululizo alipüotimua Andy Roddick wa Marekani kwa seti3: 6-2 7-6 na 6-4.Mswisi federer,anajiunga sasa na safu ya mabingwa wakubwa kama Bjorn Borg wa sweden na Pete Sampras wa Marekani –mabingwa pekee kushinda mataji 3 ya wimbledon mfulilizo tangu mchezo wa tennis kugeuka wa malipo,1968.

Upande wa wasichana,Venus Williams wa Marekani, alimtimua nae muamerika mwenzake Lindsay davenport kwa seti tatu: 4-6 7-6 na 9-7 kunyakua nae taji lake la tatu la Wimblöedon hapo jumamosi.Ilikua finali yake ya 5 ya wimbledon mnamo muda wa miaka 6.

Kati ya kura 20 na 30 hivi hazijulikani zitapigwa kwa mji gani katika kinya’ngayiro cha juamtanmo hii kuamua wapi michezo ya olimpik ya majira ya kiangazi 2012 itafanyika.Macho yanakodolewa juu ya ama London au Paris.Miji mingine inayoania ni Madrid,New York na Moscow.Wajumbe 116 wa IOC watapiga kura huko Singapore,jumatano .

Katika mbio za baiskeli za Tour de France,Lance Armstrong wa Marekani,bingwa mara 6 wa mbio hizi amenaza uzuri kuania taji lake la 7.Armstrong ameibuka wapili katika hatua ya kwanza ya Tour de France. Kwani,Armstrong alimpiku hasimu yake mkubwa Jan Ullrich wa Ujerumani.