1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Annan aita uchunguzi katika mradi wa mafuta kwa chakula

20 Machi 2004
https://p.dw.com/p/CFeV
NEW YORK: Kufuatana na shutuma za ulaji rushwa katika ule mradi kuhusu ‚mafuta badala ya chakula' nchini Iraq, Katibu Mkuu wa UM Kofi Annan ametangaza utafanyika uchunguzi huru wa daraja ya juu kabisa. Bwana Annan alitoa mwito wa kufanywa uchunguzi huo katika hati aliyolipelekea Baraza la Usalama la UM. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa mtawala wa zamani wa Iraq Saddam Hussein akishirikiana na makampuni ya Kimagharibi wameiba pesa biliyoni kadha za UM kwa kufanya biashara za ulaji rushwa. Inasemekana katika harakati hizo haramu za kibiashara yameshiriki makampuni kutoka Ulaya, Urusi, Uchina na Mashariki ya Kati. Pia inasemekana huenda watumishi wa UM walishiriki katika wizi huo.- Mradi huo wa "mafuta badala ya chakula' uliomalizika Novemba, uliiruhusu Iraq iuze kiwango fulani cha mafuta yake kuiwezesha kuununulia umma wake chakula na madawa.