1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANGERS : Kesi ya kufanya ngono na watoto yaanza Ufaransa

4 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFZn

Nchini Ufaransa wanaume na wanawake 66 wanaotuhumiwa kwa kuwadhulumu kingono watoto 45 wamefunguliwa mashtaka.

Zaidi ya mawakili 60 wanahusika katika kesi hiyo ambayo inatarajiwa kuendeshwa kwa miezi kadhaa.Waendesha mashtaka wanasema kwamba kati ya mwaka 1999 na mwaka 2001 madarzeni ya watoto walibakwa au kuchezewa kingono katika mji wa mgharibi ya nchi hiyo wa Angers.Wanasema ushahidi unaonyesha kwamba wazazi wamewatowa watoto wao wenyewe kwa kubadilishana na vitu kama kwa kupatiwa vijisenti kidogo,sigara na chakula.

Mahkama imetowa ushauri nasaha wa mfadhaiko wa akili kwa wajumbe wa baraza la mahkama kutokana na ushahidi kuwa na umbo la kufadhaisha.

Iwapo washtakiwa hao watapatikana na hatia watatu kati yao wanaweza kukabiliwa na hukumu ya kifo.