Karibu katika tamasha la Simiyu linalofanyika kwa mara ya pili nchini Tanzania. Jamii mbili zenye upinzani wa jadi za Wagika na Wagalo kutoka kabila la Wasukuma hushindana kutafuta mshindi katika ngoma za asili, ukulima, utibabu wa kutumia miti shamba na wingi wa watu katika kila jamii. Kila upande unapambana kuibuka mshindi. Angalia hapa mambo ya Simiyu huko nchini Tanzania.