1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amnesty yasema watu 13 wamefariki maandamano Nigeria

2 Agosti 2024

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International linasema waandamanaji 13 wameuwawa kutokana na maandamano yaliyofanyika Nigeria kupinga hali mbaya ya kiuchumi nchini humo.

https://p.dw.com/p/4j1ur
Nigeria | Maandamano ya kupinga utawala mbaya mjini Lagos
Raia wa Nigeria wakifanya maandamano kupinga ugumu wa maisha na utawala mbaya, Agosti 1, 202.Picha: Adekunle Ajayi/IMAGO/NurPhoto

Mkurugenzi wa Amnesty nchini Nigeria, Isa Sanusi, amesema kwamba wamethibitisha vifo hivyo vilivyoripotiwa na mashuhuda, familia za wahanga na mawakili. Mamlaka za Nigeria zimethibitisha watu wanne waliuwawa kutokana na bomu na mamia ya wengine kukamatwa. Maandamano hayo yalichangia kutolewa kwa amri za kutotoka nje katika miji kadhaa. Inspekta Mkuu wa polisi Nigeria amesema kuwa polisi wametakiwa kuwa macho na huenda wakaomba msaada wa jeshi kufuatia maandamano hayo ya jana yaliyogeuka kuwa machafuko. Miji mikubwa, kama Abuja na Kano, ambayo ilishuhudia machafuko jana, imekuwa na utulivu leo wakati ambapo maandamano yanatarajiwa kuendelea.