Amnesty: Wenye silaha Niger wanauwa watoto zaidi
13 Septemba 2021Matangazo
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International limesema idadi inayoongezeka ya watoto wanauwawa au kulengwa kwa ajili ya kusajiliwa katika makundi ya wanamgambo, katika machafuko yanayoendelea katika mpaka wa Niger na Mali na Burkina Faso.
Naibu mkurugenzi wa Amnesty kitengo cha kukabiliana na mizozo Matt Wells amesema makundi ya wanamgambo yamevamia shule mara kwa mara na yanawalenga watoto.
Shirika hilo limeyalaumu makundi ya kigaidi ya Dola la Kiislamu huko Sahara ISGS na kundi lililo na mafungamano na al-Qaeda la Jama'at Nusrat al-Islam wal-Muslimin JNIM, kwa masaibu yanayowakumba watoto katika eneo hilo.