1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Aliyekuwa waziri wa ulinzi Korea Kusini ajaribu kujiua

11 Desemba 2024

Aliyekuwa waziri wa ulinzi nchini Korea Kusini Kim Yong Hyun, amenusurika jaribio la kutaka kujitowa uhai akiwa rumande.

https://p.dw.com/p/4o0sV
Kim Yong Hyun, waziri wa zamani wa Ulinzi wa Korea Kusini (picha ya maktaba)
Kim Yong Hyun, waziri wa zamani wa Ulinzi wa Korea Kusini (picha ya maktaba)Picha: Celal Gunes/Anadolu/picture alliance

Kim Yong Hyun ambaye alikamatwa kufuatia  kadhia ya Rais Yoon Suk Yeol ya kutangaza amri ya kijeshi, alijaribu kujitowa uhai akiwa rumande anakozuiliwa mjini Seoul.

Anashikiliwa kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka na kubeba dhima kubwa katika uasi uliotokea.

Ofisi ya Rais Suk Yeol imewazuia polisi kuendesha msako kwenye majengo ya ofisi hiyo.

Korea Kusini bado inakabiliwa na mkwamo wa kisiasa huku chama kikuu cha upinzani cha Democratic kikishinikiza muswaada mpya wa kumuondowa madarakani Rais Yoon kufuatia hatua yake ya kutangaza amri ya kijeshi mnamo Desemba 3.

Chama hicho kilishindwa katika jaribio lake la kwanza Jumamosi iliyopita baada ya wabunge wa chama tawala kususia mchakato wa kura ya imani.