1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ajali ya lori yasababisha vifo vya watu 10

8 Aprili 2023

Watu wasiopungua 10 wamepoteza maisha leo na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya lori kuacha njia na kuwaparamia watembea kwa miguu na madereva wa pikipiki kwenye eneo moja karibu na mpaka kati ya Kenya na Tanzania.

https://p.dw.com/p/4PqCB
Mosambik | Schwerer Verkerhsunfall in Nhamatanda
Picha: Polícia da República de Moçambique

Kwa mujibu wa polisi ajali hiyo imetokea kwenye mji wa Migori pembezoni mwa barabara kuu inayoziunganisha nchi hizo mbili baada ya dereva wa lori kupoteza udhibiti wa chombo chake kutokana na hitilafu ya breki.

Mashuhuda wamesema dereva wa lori hilo lililobeba shehena ya mchele kutokea Tanzania kuelekea Kenya alipiga honi ya tahadhari mara kadhaa kabla ya kupoteza mwelekeo na kupinduka.

Kamanda wa polisi wa eneo ilikotokea ajali Mark Wanjala amesema juhudi zinafanyika kuwatoa watu wengine walionasa chini ya chombo hicho.

Soma Zaidi:Wanafunzi 8 wafariki katika ajali mkoani Mtwara, Tanzania