1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Afrika Kusini yaishtaki Israel ICJ kwa 'mauaji ya kimbari'

30 Desemba 2023

Afrika Kusini imewasilisha kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) dhidi ya Israel kwa kile ilichokitaja kuwa vitendo vya "mauaji ya kimbari" katika ukanda wa Gaza

https://p.dw.com/p/4aige
Kikao cha Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) wakati wa kusikiza kesi ya Ukraine dhidi ya Urusi iliyoanza Juni 6-14, 2023
Kikao cha Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ)Picha: Wiebe Kiestra/UN

Kwa mujibu wa taarifa, kesi hiyo katika ICJ inahusiana na madai ya ukiukaji wa Israel wa jukumu lake chini ya Mkataba wa Mauaji ya Kimbari, na kusema kuwa "Israel imejihusisha, inajihusisha na inatishia kushiriki zaidi katika vitendo vya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina huko Gaza".

Afrika Kusini yasema Israel inalenga kuwaangamiza Wapalestina Gaza

Katika kesi hiyo, Afrika Kusini pia inasema Israel imekuwa ikichukuwa hatua '' kwa lengo la kuwaangamiza Wapalestina katika Ukanda wa Gaza kama sehemu ya kundi pana la taifa, rangi na kabila la Palestina''.

Majengo yalioharibiwa na shambulizi la Israel mjini Rahaf Kusini mwa Ukanda wa Gaza mnamo Desemba 29, 2023
Majengo yalioharibiwa na shambulizi la Israel katika Ukanda wa GazaPicha: AFP/Getty Images

Israel yapinga mashtaka dhidi yake

Israel imepinga mashtaka hayo, huku msemaji wa wizara yake ya mambo ya nje Lior Haiat akiandika kwenye ukurasa wa X, ambao awali ulijulikana kama twitter kwamba  "Israel inakataa na kuchukizwa na kashfa inayoenezwa na Afrika Kusini na ombi lake''  kwa mahakama ya ICJ.

Soma pia;Israel yaongeza mashambulizi ya anga na ardhini Gaza

Vita hivyo vilivyofuatia mashambulizi makali ya kundi la wanamgambo wa Hamas dhidi ya Israel vinakaribia wiki yake ya kumi na mbili, huku maeneo makubwa ya Kaskazini mwa Gaza yakiharibiwa na mashambulizi ya anga ya Israel na mapigano ya ardhini yanayolenga wilaya za Kati na Kusini mwa ukanda huo.