1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya dola Mil.800 kutolewa Afrika kukabiliana na Mpox

27 Septemba 2024

Zaidi ya dola milioni 800 ndizo zilizoahidiwa kwa vituo vya kudhibiti na kuzuia magonjwa barani Afrika ili kupambana na mlipuko wa Mpox.

https://p.dw.com/p/4l99x
Chanjo ya Mpox
Chanjo ya MpoxPicha: Maule/Fotogramma/ROPI/picture alliance

Zaidi ya dola milioni 800 ndizo zilizoahidiwa kwa vituo vya kudhibiti na kuzuia magonjwa barani Afrika ili kupambana na mlipuko wa Mpox.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kituo cha kuzuwia na kudhibiti magonjwa barani Afrika (Africa CDC) Jean Kaseya ambaye ameongeza kuwa kiasi hicho ni kikubwa kuliko kiasi kilichotarajiwa cha dola milioni 600.

Soma: Chanjo za ugonjwa wa Mpox zaanza kutolewa Afrika

Ugonjwa wa Mpox uliofahamika awali kama homa ya nyani ulitangazwa mwezi Agosti kuwa dharura ya afya duniani, baada ya aina mpya kuanza kuenea kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hadi kwenye mataifa jirani. Tangu kuanza kwa mwaka huu, Afrika imeshuhudia visa zaidi ya 32,000 na vifo 840.

,