Vitendo vya ukatili wa kijinsia majumbani vimeendelea kutikisa huku wenza wakifanyiana visa vinavyosababisha wakati mwingine vifo, ulemavu na uharibifu wa mali. Mfano ni kisa kilichotokea huko Mtwara ambapo mwanamke mmoja alinusurika kifo baada ya mumewe kuichoma nyumba ya familia kisa ugomvi. Salma Mkalibala alimtembelea mwanamke huyo kusikiliza simulizi yake.