1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA. Rais Obasanjo awafuta kazi mawaziri wake.

5 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFQ8

Katika kampeni yake dhidi ya ufisadi, rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria amemfuta kazi waziri wa pili katika kipindi cha muda wa chini ya majuma mawili. Waziri wa ujenzi, Alice Mobolaji Osomo, ametimuliwa kufuatia kuzuka kwa kashfa juu ya njama yake ya kuwauzia maafisa wakuu wa serikali na jamii zao mali ya umma. Muda mfupi kabla kumtimua waziri huyo, rais Obasanjo alimfuta kazi wazri wake wa elimu na kuwalaumu hadharani wabunge wakongwe, akiwemo spika wa bunge, kwa kupokea hongo ili waipitishe bajeti ya mwaka huu. Wakati huo huo, waongoza mashtaka wamemshitaki mkuu wa polisi kwa kuiba euro milioni 77 wakati alipokuwa madarakani kwa muda wa miaka mtatu. Tafa Balogun aliyakanusha mashtaka yote 70 yaliyowasilishwa dhidi yake. Nigeria imeorodheshwa taifa la tatu duniani kwa ulaji rushwa na shirika la rushwa la Transpareny International.