1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA: Mkuu wa Benki ya Dunia ziarani Afrika

12 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF4H

Rais mpya wa Benki Kuu ya Dunia,Paul Wolfowitz amewasili Nigeria,akianza ziara yake ya wiki moja barani Afrika.Alipowasili Abuja,alisifu uamuzi wa kundi la G-8 la madola manane tajiri,kuzisamehe nchi zilizo masikini sana madeni yake.Nigeria yenye madeni makubwa haihesabiwi kama nchi masikini kwa sababu ya pato lake la mafuta.Siku ya jumatatu,Wolfowitz atakutana na rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria na atatembelea pia vituo vya afya.Kabla ya kuikamilisha ziara yake siku ya jumanne nchini Nigeria,Wolfowitz atakutana na wafanya biashara,wakulima na maafisa wa serikali.Ziara hii itampeleka pia Burkina Faso,Rwanda na Afrika Kusini.